Mbatia achukuliwa fomu ya Ubunge ya kuwania ubunge Jimbo la Vunjo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha  NCCR-Mageuzi Jimbo la Vunjo, kwa kauli moja wamechanga fedha kiasi cha Sh 370,000 na kumchukulia fomu Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake James Mbatia kwa ajili ya kugombea ubunge kwa kipindi kingine 


Mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Mbatia ameahidi kuwa atafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha maendeleo ya Jimbo hilo yanazidi kukua kwa kasi, na kuahidi kuwatumikia wananchi wa Jimbo hilo kwa nguvu zake zote. 


''Kutoka sakafu ya moyo wangu ,nabeba dhamana  ya kugombea Ubunge wa Jimbo hili la Vunjo ,naahidi tutafanya kazi kwa pamoja usiku na mchana ili kutimiza yale yote ambayo mnayatamani yafanyike" amesema Mbatia. 


Aidha ameongeza kuwa, "Vunjo ni yetu na niahidi kuwa Vunjo yetu itaendelea kung'ara na yale machache ambayo hatukuyakamilisha kutokana na changamoto za hapa na pale tutaenda kukamilisha". 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad