7/23/2020

Mchanganyiko Huku Mwili wa Marehemu Wadinda Kusafirishwa Nyumbani kwa MazishiMwanawe alimnunulia jeneza la kifahari baada ya kumtelekeza na kufa kwa umasikini. Picha: Hisani

Mwili wa marehemu Nasimiyu ulikataa kusafirishwa nyumbani Kakamega kufanyiwa mazishi

Marehemu alikuwa na wana wawili, wa kiume na wa kike

Mwanawe alimnunulia jeneza la kifahari baada ya kumtelekeza na kufa kwa umasikini

Kilitokea kisa cha kushangaza huku maiti akidinda kusafirishwa hadi nyumbani kwa mazishi kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Kulingana na kisa hicho kilichofanyika katika mji wa Kisumu, marehemu alifura kupita kiasi na hakuweza kuingia kwenye jeneza la kifahari alilonunuliwa na mwanawe.

Jarida la Bongo Leo limebaini kuwa marehemu alijaliwa wana wawili, wa kike na wa kiume. Mwanawe wa kiume alijaliwa maishani na kupata donge refu Nairobi na kumuacha mamake akiishi katika maisha ya umaskini Kisumu hadi kifo chake.Kulingana na tamaduni za Kiluhya, baada ya marehemu kukataa kuingizwa katika jeneza la kifahari, mwanawe wa kike alichanga fedha na kununua jeneza jingine la kawaida kisha akakubali kuingizwa humo.

Mwanawe wa kiume alileta magari 20 ya kifahari baadaye kusafirisha mwili wa mamake hadi nyumbani, baada ya jeneza hilo kupakiwa ndani ya gari, gari lilizima kabisa, na kila jeneza lilipotolewa, liliweza kunguruma.

Wenyeji walifanya tambiko na kumshauri mwanawe wa kike kutafuta gari jingine, alileta gari la kusafirisha mbao, mwili ulikubali na kusafirishwa hadi Kakamega kwa mazishi. Mwanawe wa kiume alisalia kwa aibu na masikitiko kwa kumteleke mama mzazi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger