Meek Mill Ashtakiwa kwa Kuiba Mashairi


RAPA  Meek Mill amefunguliwa mashtaka kwa kuiba mashairi ya nyimbo mbili za lebo ya Philadelphia.

Kampuni ya Dream Rich Entertainment imefungua mashtaka hayo dhidi ya Meek  mwezi uliopita ikiishitaki lebo yake ya utoaji nyimbo ya Dream Chasers na kampuni-mama yake ya Atlantic Records kuhusika katika wizi huo.

Dream Rich inasema kwamba Meek aliiba mashairi hayo katika nyimbo zake za  “100 Summers” na “Cold Hearted II” akijifanya ni zake.

Huko mahakamani, imesema Mek aliyapata mashairi hayo na kuyaingiza katika albam yake ya mwaka 2018 iliyoitwa Championships. That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments