Membe “Sitakuja Kurudi CCM tena”


Undani wa Bernard Membe kung'olewa - MtanzaniaAliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe amesema hawezi hata siku moja kurudi ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kama watu wengi wanavyozani.

Akizungumza kwenye mahojiano ya moja kwa moja na muandishi wa habari mkongwe nchini Jenerali Ulimwengu amesema CCM ndiyo imemkataa na si yeye ndiyo maana walimfukuza kwenye chama hicho.

“Chama cha mapinduzi ndo kimenikataa na kunifukua uwanachama sio mimi sikikukataa chama cha mapinduzi sasa nasema hivi hutanisikia tena nikirejea ndani ya CCM” amesema Membe.

Ikumbukwe kuwa Membe amekuwa akihusishwa na kujiunga na vyama vingine vya siasa nchini ili kutimiza ndoto ya kuwa rais wa Tanzania.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments