7/16/2020

Membe “WanaCCM Wengi Hawana Furaha”


Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje Bernard Membe amesema kuwa chama chake  za zamani CCM kinapaswa kujipanga kuelekea kwenye uchaguzi unaokuja kwani wapo wanaccm wengi watakaotafuta furaha nje ya chama hicho.

Akizungumza kwenye mahojiano ya maalum na mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu kwenye kipindi maalum kwenye televisheni mtandao ya mwandishi huyo Membe amesema anamini wapo wengi ambao hawana madaraka na wamechoka kuwa bila furaha.

“Mimi napata nguvu kubwa kuwa kuna watu wengi sana ambao ni wanachama wa kawaida wengi ndani ya CCM ambao wanataka uhuru, wanataka furaha na wataunga mkono juhudi za kusaka furaha hiyo nje kwakua wameikosa ndani ya CCM yao ndani ya miaka 5” amesema Membe.

Ikumbukwe Bernard Membe anatarajiwa kutangazwa muda wowote kujiunga na chama cha ACT wazalendo ili kuweza kutikiza ndoto yake ya kugombea urais.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger