7/26/2020

"Mkapa Alinifanya Nianze Kupiga Kura" - Shusho


Msanii wa nyimbo za Injili Tanzania Christina Shusho amesema moja ya matukio anayoyakumbuka kutoka kwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa ni kupiga kura kwa mara yake ya kwanza na alivyotangaza kifo cha Baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.Akizungumza kwenye show maalum ya Friday Night Live Christina Shusho amesema

"Kikubwa ninachokikumbuka wakati wa uongozi wake kwa mara ya kwanza nikaanza kupiga kura kumbukumbu hiyo hainitoki nashukuru Mungu ni baraka, amefanya vizuri na tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake, nakumbuka tena mwaka 1999 anatangaza kifo cha Baba wa Taifa kwa wakati huo ilikuwa ngumu kwa sababu tulikuwa tuna hofu ya kuingia mwaka 2000 maana tuliambiwa Yesu anarudi kutakuwa na mabomu, mlipuko na radi" ameeleza Christina Shusho 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger