Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mke Aeleza Alivyozichapa Kavukavu na Chege

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREKUMEKUWA na kawaida ya mastaa wa fani mbalimbali kutodumu muda mrefu kwenye mahusiano yao kutokana na sababu mbalimbali na kitu kikubwa zaidi ni kutokana na ustaa walionao, ambao unasababisha mambo mengi kutokea kwenye mahusiano yao ya kimapenzi.


 


Vitisho vya kuvunjika mahusiano ya kimapenzi ya mastaa, havimtetemeshi kabisa Zahara Said, ambaye ni mke halali kabisa wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Said Hassan ‘Chege Chigunda’ ambaye wapo pamoja kwa takriban miaka minne na tayari wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Jada.


 


Bibie huyo anajiamini kwa asilimia mia kuwa Chege hakohoi kwake, tumsikilize hapa amefunguka mambo mengi kuhusu maisha yao kwa ujumla:


 


Mikito: Hongereni kwa wimbo mzuri wa Mama Pekupeku mliofanya na mumeo Chege.


 


Zahara: Asante sana.Mikito: Nilikuwa sijui kama na wewe ni mwanamuziki, maana umefanya vizuri sana kwenye wimbo huo…Zahara: Huwezi amini kabisa, mimi sio mwanamuziki na wala sipendi kuimba kabisa.Mikito: Ilikuwaje sasa mpaka ukaimba?
Zahara: Ni Chege ndiye aliniambia ni lazima tuimbe wote na hata nilivyomaliza kurekodi, nilijiuliza kwa nini niliimba.


Mikito: Naamini watu wengi walijua uko na Chege kwa vile unapenda muziki wake na unapenda kuimba pia.


 


Zahara: Hapana, Chege nilipendana naye yeye kama yeye na si kitu kingine chochote kile, yaani niliweka muziki wake pembeni.


Mikito: Sasa Chege ni mwanamuziki na kazi zake ni ngumu kuna wakati inabidi alale studio au hata kujichanganya na wanawake warembo, hilo wewe halikutishi?


 


Zahara: Hapana, kwanza huwezi amini, anapokuwa studio naona sawa hata kama akilala huko, lakini kingine kuhusu warembo sina shida nalo hikabisa.


 


Mikito: Mbona kama unajiamini sana?


Zahara: Lazima nijiamini kwa sababu najua kabisa Chege hafurukuti na si kwamba nimempa limbwata.Mikito: Ni nini sasa kama sio limbwata hilo?


Zahara: Unajua Chege namjua sana na yeye ananijua, hivyo tunajuana vilivyo kabisa, hakuna wa kumdanganya mwenzake na ndiyo maana tupo mpaka leo hii tunajuana kwa kweli.


Mikito: Vipi kuhusu suala la wivu, baina ya wewe na yeye?


 


Zahara: Yeye ana wivu sana, mimi naona kawaida.


Mikito: Tukio gani alilowahi kulifanya kutokana na wivu?


 


Zahara: (Kicheko) alishawahi kunipiga kisha tukapigana pale kwenye mgahawa wa Shishi Food.


Mikito: Kisa ni nini sasa?


Zahara: Ni wivu tu wa kimapenzi, sijui alihisi nazungumza na mtu basi ikatokea hivyo, lakini tuliyamaliza.


 


Mikito: Umekuwa mwanamke wa tofauti maana watu wengi hawakufahamu, lakini pia huonekani kwenye mikusanyiko mbalimbali ya mastaa.


Zahara: Ndiyo nilivyo, sipendi maisha ya maonyesho wala kujichanganya kabisa na ndiyo maana hata mtaani kwangu wengine hawajui kama ni mke wa Chege kwa sababu naishi maisha ya kawaida.


 


Mikito: Kwenye nyimbo mliyoimba na Chege ya Mama Pekupeku, mlikuwa mna maanisha nini?


 


Zahara: Ni wimbo tu wa kawaida wa maisha halisi wanayoishi watu mitaani, lakini haina maana nyingine wala kumlenga mtu yeyote.


Mikito: Una tabia ya kukagua simu ya Chege?


Zahara: Siwezi na wala haitakaa itokee, sio maisha yetu hata siku moja, kila mtu anajichunga mwenyewe siku zote, mambo ya kuchunguzana kwenye simu hapana.


Mikito: Haya Zahara nakushukuru kwa muda wako.


Zahara: Asante sanaPost a Comment

0 Comments