google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Msafara wa kijeshi wa Marekani washambuliwa kwa mabomu Iraq | UDAKU SPECIAL

Msafara wa kijeshi wa Marekani washambuliwa kwa mabomu Iraq

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msafara wa magari ya kijeshi ya Marekani umeshambuliwa kwa mabomu ya kuelekezwa kutoka mbali (VBIED) baina ya barabara ya Samawah na Diwaniyah, kusini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Duru za kiusalama zinaarifu kuwa, kwa akali magari matatu ya kijeshi ya Marekani yameharibiwa vibaya katika shambulizi hilo lililofanyika mwendo wa saa nne usiku wa kuamkia leo.
Inaarifiwa kuwa, msafara huo wa magari ya kijeshi ya Marekani ulikuwa unatoka mji wa Diwaniyah katika mkoa Al-Qadisiyyah ukielekea katika mkoa wa Svehiclein Muthanna kabla ya kushambuliwa. Kanda ya video iliyosambaa kwenye vyombo vya habari na katika mitandao ya kijamii inaonyesha namna magari hayo yalivyoteketea kwa moto baada ya shambulizi hilo.
Haijabainika iwapo shambulizi hilo limesababisha maafa mbali na kulitia hasara jeshi vamizi la Marekani lililoko Iraq. Kundi jipya la Saraya Thawrat al-Eshreen al-Thaniya limetangaza kuhusika na shambulizi hilo la jana usiku.



Upinzani dhidi ya uwepo wa askari vamizi wa Marekani nchini Iraq ulishtadi tokea Januari mwaka huu, baada ya jeshi la kigaidi la US kuwaua kikatili aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Naibu Kamanda wa harakati ya wananchi wa Iraq ya Hashdu Shaabi, Abu Mahdi al-Muhandis katika mji mkuu Baghdad.
Baada ya jinai hiyo, Bunge la Iraq mnamo Januari 5 lilipasisha muswada wa sheria ya kutaka kuondoka nchini humo majeshi yote ya kigeni.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad