Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Msanii Size 8 afichua "Sikuwa Navaa Chupi Kabla ya Kuokoka"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURELinet Munyali, maarufu kama Size 8, amewaacha mashabiki wake wamechangamka baada ya kuwafichulia siri zake kabla ya kuokoka.

Size 8 alisema kuna mambo alikuwa akiyafanya kabla ya kuona uzima wa Bwana ambayo kwa sasa hawezi.


Size 8 aliokoka na anasema maisha yake yalibadilika pakubwa.

Kwenye mahojiano na redio Maisha, Size 8 alisema enzi zake katika maisha ya kidunia alikuwa akifurahia kupata upepo mwembamba.

"Ni kweli, nilikuwa nuikitembea siku hizo bila chupi," alisema msanii huyo.

Size 8 aliwacha usanii wa nyimbo za raha na kuingia nyumba ya Bwana. 

Aidha wakati uo huo alipuuza madai kuwa ndoa yake na DJ MO imeingia doa kwa sasa akisema wanafurahia penzi lao.


"Maisha ya ndoa yangu ni matamu. Tunayafurahia sana," alisema lakini akaongeza kuwa ako katika kipindi cha kiu cha penzi la nyuma ya pazia.

Kwenye mahojiano na redio Maisha, alisema maisha yake yamebadilika sana.

Katika maisha yake ya kupiga mtindi, kipusa huyo alisema hakuna wakati alizidiwa kiwango cha kumpigia simu mmoja wa waliokuwa wapenzi wake.


"Sijawahi kulewa kiwango cha kumpigia mmoja wa waliokuwa wapenzi wangu. Kiburi changu hakingeniruhusu kufanya hivyo," alisema.

Post a Comment

0 Comments