Mtoto wa Mandela Aliyefariki Alikutwa na Corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Zindzi Mandela, mwana mdogo wa kike wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela na mwanaharakati wa kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi, Winnie Madikizela Mandela alikutwa na virusi vya corona.

Alifariki katika hospitali ya mjini Johannesburg mapema siku ya Jumatatu akiwa na umri wa miaka 59.

Mwanawe Zondwa Mandela aliambia chombo cha habari cha Afrika Kusini SABC kwamba haijulikani iwapo ni ugonjwa huo uliosababisha kifo chake.

Familia inasubiri ripoti ya uchunguzi.

”Ni kweli kwamba alikutwa na virusi vya corona hivyobasi ni vyema kufanyakazi chini ya masharti yaliopo ya kukabiliana na maradhi hayo”, alisema Zondwa Mandela.

 

Unaharakati na siasa
Mwanamke huyo alikuwa mwanarakati wa kisiasa na ni miongoni mwa wale waliopigana dhidi ya uongozi wa ubaguzi wa rangi nchini humo.

Alianza kuhudumu kama balozi wa Denmark mwaka 2015.

Alikua mwana wa sita wa Nelson Mandela na wa pili kati yake na Winnie Madikizela Mandela.

Wakati alipokuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi sita babake, alifungwa jela. Mamake pia alifungwa mara kwa mara wakati huo.

Mwaka 1977 Madikizela Mandela alipelekwa katika eneo la Brandfort, katika jimbo la Orange Free State na Zindzi aliandamana naye.

Baadaye alielekea nchini Swaziland na alipokamilisha shule ya upili, alijiungana na Chuo kikuu cha Cape Town kwa shahada ya sheria.

Mwaka 1985, aliofuzu . Zindzi alichaguliwa kusoma taarifa ya babake ya kukataa kutoka jela baada ya aliyekuwa rais wa taifa hilo PW Botha kumtaka kutoka jela bila masharti.

Wakati babake Nelson Mandela alipotoka jela 1990, mazungumzo yalianza kati ya chama cha ANC na utawala uliokuwepo kufutilia mbali mfumo wa ubaguzi wa rangi.

Huku Afya ya aliekuwa rais wa ANC ikizorota , Mandela alichaguliwa kama raia mpya wa Chama cha ANC na mgombea wa urais nchini Afrika kusini katika uchaguzi wa 1994.

Baada ya Mandela kuchaguliwa rais na kumpatia talaka mkewe Winnie 1996, Zindzi alichaguliwa kuandamana na babake katika sherehe ya kumuapisha.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad