Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mtoto wa Will Smith Aitwa Jaden Afunguka Sababu za Kuacha Kutumia Jina la Baba yake Mzazi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Achana na Banana pamoja na Maunda ambao waliamua kutumia jina la baba yao [ZORO] kwenye majina yao kamili ya muziki, Jaden na Willow hawakufanya hivyo.

Willow alianza kutambulika kimuziki kabla ya Jaden, na alianza kwa kujiita [Willow Smith] na baadaye kuliondoa jina la baba yake. Hii ni moja kati ya vitu ambavyo vilimvutia pia Jaden ambaye mwaka jana alitangaza kuacha kujiita [Jaden Smith] na kutumia Jaden pekee kwenye muziki wake.

Kwenye mahojiano na Zane Lowe wa Apple Music, Jaden amefafanua kwa nini alichukua maamuzi hayo. Amesema lengo ni kuweka utofauti kwenye kazi, kwa sababu Jaden Smith atakuwa akicheza filamu na Jaden atakuwa akiimba muziki. Hiyo itamfanya shabiki kutochanganya mambo.

Post a Comment

0 Comments