Mwanamke Akiri Kumdunga Kisu Mumewe Kufuatia Mabishano ya Meseji iliyoingia Kwenye Simu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Anaidaiwa kukimbia jikoni na kuchukua kisu kabla kumdunga mumewe kifuani na kumsukuma ukutani. Hisani.

Mwanamke aliyekamatwa na kufikishwa kortini baada ya kumdunga mumewe kisu tumboni wakikangangania simu amekiri makosa na kujitetea.

Mary Nduta alikiri kumdunga kisu mumewe Solomon Njoroge  Maingi  nyumbani kwao katika mtaa wa Mwiki, Kasarani Nairobi Julai 19.

Akizungumza mbele ya hakimu mkazi David Ndungu katika mahakama ya Mlimani, Nduta alieleza kuwa alimdunga kisu mumewe kama njia ya kujikinga baada ya kuzidiwa nguvu.

Mlalamishi, Solomon Njorogo Maingi anaendelea kupata matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta alikolazwa baada ya mkasa huo.

Njoroge alirudi nyumbani baada ya wiki mbili na mkewe kuanza kulalamika kuhusu jinsi mumewe wa kwanza alivyokuwa akimpa pesa nyingi kumshinda..

Njoroge alijua kuwa alikuwa katika mawasiliano na mume huyo na hivyo akataka kuona simu, hapo ndipo majibizano yalianza .

Nduta anaidaiwa kukimbia jikoni  upesi na kuchukua kisu kabla kumdunga mumewe kifuani na kumsukuma ukutani.

Njoroge aliokolewa na jirani ambaye alifika upesi na kumtolea kisu hicho kifuani kabla kumkimbiza hospitalini kwa matibabu.

Mwanamke huyu alinaswa na maafisa wa polisi waliopata kisu pamoja na nguo ya kulala katika chumba chao cha kulala zikiwa na matome ya damu.

Nduta aliachiliwa kwa dhamana ya KSh 100,000 huku kesi yake ikisubiriwa kutajwa tena Agosti 4, 20202.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad