7/25/2020

Mwanamke Mwenzangu, Usigombane na Mwanamke Mwenzako Kisa ni Mchepuko wa Mume Wako

Mimi kuna kitu huwa siwezi kabisa kukifanya, nimkute mwanaume wangu na mwanamke mwingine, sitomfanya chochote kabisa.

Kwani yeye amefwatwa kama mimi alivyonifata akanitongoza tu.Sasa iweje nianze kupigizana kelele na mwanamke mwenzangu.

Nitakachofanya ni kupambana na mwanaume tu. Yeye ndo atakuwa haniheshimu mpaka anaenda kumfata mwanamke mwingine.

Utakuta mwanamke anapigizana makelele na mchepuko wa mume wake, utafikiri alimfata mume wako akamwambia naomba unifanye mchepuko.

Pambana na mume wako.Mimi kuna mwanamke alinifata nilikuwa simfahamu kabisa na wala sijawahi kutembea na mume wa mtu.

Nilitukanwa matusi mazito mpaka nikashangaa, aliniudhi sana. Nikakaa nikafikiria nimfanyaje ili aumie. Nikamwambia, kwa vile nimekujibu kistaarabu mimi sitembei na mume wako ukanitukana, sasa basi ndo mda wa kumkubalia rasmi, maana alikuwa ananitongozaga mda tu.

Na ahadi alizoniahidi ngoja nikubali azitekeleze. Baada ya kusoma SMS, alipiga simu anaomba msamaha na maneno kibao. Alichoambulia ni too late na block juu. Alihaha kupiga na simu nyingine mpaka alichoka. Huku namcheka tu.

By Super women 2

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger