7/29/2020

Mwanamuziki DRAKE Aweka Rekodi Hii ya Muda Wote Billboard

Drake ameendelea kuweka rekodi za kutosha kwenye chati za Billboard Hot 100, wiki hii ameweka hii kubwa ya muda wote.

Rapa huyo toka Toronto, kwa sasa ndiye msanii mwenye maingizo mengi zaidi kwenye Top 10 ya chati hizo kwa muda wote. Amefikia mafanikio hayo mara baada ya nyimbo mbili alizoshirikishwa na DJ Khaled "Popstar" na "Greece" kuingia kwenye chati wiki hii na kumfanya kuwa na maingizo 40.

Drake amempiku Madonna ambaye kwa sasa amebaki na maingizo 38 kwenye chati hizo zenye umri wa miaka 62.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger