Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mzee yusufu arudi rasmi kwenye muziki wa taarabu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Unakumbuka Machi 12, 2020, MzeeYussuf alipowashtua wengi pale alipoandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa anarudi mjini na ataimba mpaka agalegale.

 Jambo hilo halikuwashtua tu mashabiki bali na baadhi ya viongozi wa dini kutokana na msanii huyo kuamua kujikita katika masuala ya dini. 

Pamoja na kuhojiwa mara kwa mara kuhusu kauli hiyo hakuwahi kusema kuwa anarudi kwa staili gani hadi leo Jumatano Julai 22, 2020 kuweka tangazo (pichani) katika ukurasa wake wa #Instagram na kueleza tukio la uwepo wake katika viwanja vya Dar Live, tukio aliloliita 'Mzee Yussuf anarudi Mjini'. 

Katika tangazo hilo ameeleza pia wasanii wa taarabu watakaomsindikiza kuwa ni pamoja na mke wake #LeylaRashid, dada yake #HadijaYussuf, wengine ni #FatmaMcharuko, #PrinceAmigo na Mtoto Pori. 

Mwisho wa tangazo hilo ameweka maneno yaliyosomeka, "Mungu pekee mwenye mamlaka na mimi na atanibariki Amin". 

Kupitia tangazo hilo ni wazi kwamba sasa MzeeYussuf aliyewahi kutamba na nyimbo mbalimbali zikiwemo “Mpenzi Chocolate”, “Daktari wa mapenzi”, “Nitadumu Naye” na “VIP” anaweza kuja na sapraizi kwa mashabiki zake.

Post a Comment

0 Comments