7/27/2020

Nasubiri Kumfumania Mke Wangu, Naombeni Ushauri

Waku habari za mchana,kama nilivyojieleza hapo juu,ni kwamba nilibahatika kuoa miaka 10 iliyopita iliyopita,tulipata sakrament ya ndoa takatifu tar.7/5/2011.pia katika ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto 2.sasa kilichonifanya nije hapa jukwaani ni taarifa nilizozipata toka kwa jirani yangu ambae amenithibitishia kuwa mke wangu anatembea na mtu ambae pia ni jirani yetu kabisa.mke wangu huwa anashinda nyumbani akijishughulisha biashara ya kiduka tulichokifungua karibia mwaka sasa.pia mimi huwa nashinda kibaruani kwangu ambapo mara nyingi huwa nachelewa kurudi nyumbani kutokana na kabiashara kangu kanakonipatia riziki.huyu jirangu kanijulisha huwa wanatoka majira ya saa 1 jioni na kurudi sa 2:30 jioni kabla mimi sijarudi.baada ya kupata tarifa hizi nilijaribu kufanya uchunguzi na nimeanza kuona kuna ukweli juu ya jambo hili.juzi ilipofika saa 1:30 jioni nilimpigia simu kumuulizia jambo fulani nikasikia anaongea taratibu tofauti na siku nyingine,nikamuuliza umeshafunga duka?akanijibu ndio,nikamuuliza mbona mapema akasema kuna mkanda nimeupenda nauangalia..nikakata simu nikampigia yule jirani kumuuliza kama mke wangu yupo nyumbani akasema hayupo na ametoka na jamaa kama kawaida yake,kama huamini uje uone.nilitamani kwenda lakini nilishindwa kujua ni uamuzi gani nichukue kwa sababu,kwanza sikujua wamekwenda guest gani,huyo jamaa anausafiri hivyo wanauwezekano wa kwenda nje ya mji kidogo.nilijikaza sikumuuliza wala kumwonyesha dalili zozote za kufahamu mambo hayo machafu anayoyafanya mke wangu.hivyo naombeni ushauri wenu pindi nikiwafumania au kuwahi kurudi home na kumkosa mke wangu wakati amenijulisha yupo home..naombeni ushauri wenu ni uamuzi gani naweza kuchukua ukawa sahihi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

9 comments:

 1. kipenzi cha wamama18 June 2014 at 14:47

  Huyoanayekuambiamanenohayo inatakiwa umuagalievizuri anaweza kukupiga changa

  ReplyDelete
 2. SIKILIZA MOYO MDOMO NI WA MAAMUZ TU

  ReplyDelete
 3. fanya uchunguzi wa kina ili upate uhakika isije ikawa huyo jirani hawatakii mema na kama utakamilisha uchugnguzi ukajua ni kweli hapo ndipo utapata uwamuzi kwani kama mkeo anatoka nje ya ndoa huyo sio mwaminifu kumbuka siku hizi kuna magonjwa ya kuambukizwa hapo unachotakiwa kwanza wewe jaribu kumwambia mukapime kama atakubali hapo majibu ndio yatakupa jibu la maamuzi kama mtakutwa wote ni wazima nikumshukuru mungu na hapo ndipo utaanza mazungumzo naye nakumuuliza kama anaichukuliaje ndoa yetu majibu ya mkweli utayapata hapo wakati akikujibu pia ujaribu kumuonya kwa hiyo tabia anayoifanya

  ReplyDelete
  Replies
  1. Yap!!Huu ndo ushauri mkuu...usipaniki fanya uchunguzi ukigundua chukua hatua ya kum4 saro wife!!over

   Delete
 4. Wewe. Ukageee hapo hapo ukisuburi kumfumania. Itasubiri sanaaa

  ReplyDelete
 5. Utasubiri sanaa

  ReplyDelete
 6. hahaha mbona atasubiri sana, fanya uchunguzi wa kina hata kwenye simu yake, mbona utamshika soon, usifanye papara kabisa na kama ukifanikiwa kumkamata, bac sema nae usione, soo. and je wewe hutoki nje ya ndoa au ndo mwanamke anaonekana kutoka nje ya ndoa kwa kuwa mwanamke, wewe huna nyumba ndogo kweli, or unachelewa kutoka kibaruanipengine ndo kwenye nyumba ndogo kweli kama huna nyumba ndogo bac ni sawa ukimfumania lkn kama na wewe unanyumba ndogo utakuwa umemuonea hahaha habari ndo hiyo

  ReplyDelete
 7. Duh una roho ngumu uliambiwa kabisa wametoka na ukamezea!kuwa mwanae bwana act soon ksbla mambo hayajaharibika!weka mtego faster na ukimfumania mchomoe....ukimsamehe moja asali haonji mara moja!

  ReplyDelete
 8. Usimwamani 100% inawezekana huyo jamaa alikuwa anamtaka, akamukataa akanza kuona wivu au anaweza kuwa msamaria mwema ila fanyauchunguzi kufanya uchunguzi itakugarimu pesa kama kukondi pikipiki kufuatilia nyendo zane, kama kufunga duka, kucheki simu yake bila yeye kujuwa kuwa una chunguza, kama inapassword kwa nini? je face book mazungumuzo ni yapi? tulia tuli kama simwaminifu itamushika.

  ReplyDelete

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger