7/14/2020

Ndinga Jipya la Zari Lamtoa Povu Tanasha


JAMBO limezua jambo! Mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna, ametoa povu, kisa ndinga jipya la Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Hii ni baada ya Zari aliyezaa na Diamond au Mondi kuongezewa pesa za kununulia gari hilo la kisasa aina ya Bentley Continental GT, lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300 za Kitanzania.

Baada ya Zari aliyezaa watoto wawili na Mondi kulimiliki gari hilo, alimshukuru jamaa huyo ndipo mashabiki mitandaoni wakaanza kumshambulia Tanasha wakimwambia aliamua kuondoka na sasa mwenzake anafaidi.

“Tanasha kwa sasa anajuta maana aliamua kuondoka na kuacha Toyota Prado (gari alilonunuliwa na Mondi) akijimwambafai kuwa ana magari mengi, sasa kiko wapi, ona mwenzake kapigwa na gari la maana,’’ alisema shabiki mmoja akimtagi Tanasha.

Tanasha ambaye amejaaliwa mtoto mmoja wa kiume na Mondi, Naseeb Junior, hakutaka kuendelea kuchafuliwa, ndipo akaibuka na povu kama lote kuwa siku zote watu wanapenda kukosoa wenzao na hawajui wanayopitia.

“Siku zote watu ambao mara zote kazi yao ni kukosoa au kukashifu watu, hawajui ni maumivu kiasi gani wanayapata.

“Elewa huu ni ukweli, siku zote watu wenye furaha na mafanikio hawana sababu ya kuwaweka wengine chini,’’ aliandika Tanasha kwenye Insta Story.


Hii si mara ya kwanza kutokea, kwani hata Zari aliwahi kuwashambulia wambeya kuwa wasimseme maana yeye hawajui na wao hawamjui.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DAR
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger