7/18/2020

Polisi Anaswa Baada ya Kufumaniwa Akimbaka Mgonjwa wa Covid19 Kwenye Karantini


Polisi wamemkamata na kumzuilia afisa mmoja wa polisi ya magereza aliyenaswa akifanya tendo la ndoa na mwathiriwa wa covid 19 aliyetiwa karantini.

Afisa huyo anayefanya kazi katika gereza la Busia alifumaniwa na maafisa wenza mwendo wa 3am katika chumba hicho cha karantini baada ya wagonjwa wengine kutoa habari.

Ripoti ya polisi katika kituo cha Busia imebaini kuwa afisa huyo alipokonywa bunduki yake kabla kutiwa karantini kwenye kituo hicho baada ya kisa hicho kuripotiwa.

Inadawa kuwa polisi huyo alikuwa katika opareshini ya usiki pamoja na maafisa wengine lakini akabaki kuzungumza na mgonjwa huyo huku wenzake wakielekea katika chumba chao maalum cha kushikia doria.


Alichukua muda mrefu na maafisa hao wengine waliporuda hapo kuangalia aliko, hakuwepo tena.

Baadaye, walisikia kamsa kutoka katika wadi ya kina mama na walipofika hapo, waliwapata wagonjwa hao nje wakilalamika kuwa mmoja wao alikuwa akibakwa na afisa wa polisi wa magereza.

Maafisa katika wizara ya afya walipashwa habari kabla kufika muda mfupi baadaye na kumtia karantini kabla ya kumpokonya bunduki yake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger