7/29/2020

Polisi Walivyozuia ndoa ya Mwanafunzi Katavi


Jeshi la polisi mkoa wa katavi limewakamata watuhumiwa 15 wakiwemo wazazi wawili kwa kumwozesha mwananfunzi wa darasa la tano anayesoma shule ya msingi ya Kaseke iliyopo manispaa ya Mpanda kwa mahari ya ngombe 12.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amesema katika mohojiano na watuhumiwa hao jeshi liliweza kungundua mbinu ya udanganyifu waliyoitumia kwa kuwaweka wahusika wawili, Stela Paul (20) na Samsoni Charles (23) kama wanandoa.

Kamanda Kuzaga amesema jeshi la polisi lilifanikisha kuisambaratisha ndoa hiyo ya kimila huku likiendelea na juhudi ya kumtafuta muoaji aliyetoroka .

Aidha kamanda kuzaga amesema jeshi halitosita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu au kikindi cha watu na kuwafikisha Mahakamani.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger