google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Q Chillah Amefunguka Sababu za Kuacha Kufanya Kazi na Harmonize | UDAKU SPECIAL

Q Chillah Amefunguka Sababu za Kuacha Kufanya Kazi na Harmonize

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Q Chillah amezungumza sababu za kuacha kufanya kazi na Harmonize ambaye mwaka jana alitangaza kumrudisha mwimbaji huyo mkongwe wa bongo fleva.

Kwenye mahojiano na XXL Clouds FM, Chillah amesema @harmonize_tz alikuwa na upendo wa kweli na nia nzuri tu lakini uongozi wake ulikuwa na tatizo, hivyo kupelekea kuchelewa kwa kazi zake kiasi cha kumfanya ajitoe kwenye mwamvuli huo

"Harmo alikuwa na upendo wa kweli, na alimaanisha kile alichokiwa anakifanya. Lakini Hamo pia si ana timu nyuma? Sasa huwezi kujua timu imemuambia nini. Muda mwingine unaona kuna ucheleweshaji wa kazi zako na wewe unapata uvivu wa kutokwenda studio kwa sababu mimi sikuwa msanii wa kwenda kusubiri studio." alisema Chillah ambaye kwa sasa anafanya kazi na Maco Chali wa MJ Records.

Kukazia tena, Chillah amesema "Mwisho wa siku Harmonize ni kijana mwelewa na anajielewa lakini hizi menejimenti nyuma ndio muda mwingine zinakuwa na maoni mengi, taarifa nyingi sana." alisema Q Chillah ambaye chini ya Harmonize aliachia nyimbo kama Nionyeshe na Go Low.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad