7/30/2020

Rais Magufuli apewa jogoo na Wanasomanga "Mpelekee mama kuku huyu mwambie asante kwa malezi aliyokupa"Mwananchi wa Somanga amemzawadia Rais Dkt. John Magufuli jogoo na kumuomba Rais ampelekee mama yake mzazi. 


"Mpelekee mama kuku huyu kutoka kwa wananchi wa Somanga, mwambie asante kwa malezi aliyokupa, uko vizuri Mhe. Rais, piga kazi." 


Baada ya hapo Rais JPM aliomba akabidhiwe Jogoo alopewa na Mzee Huyo " "Mzee nipe kabisa jogoo wangu uliyenizawadia niondoke naye, nitampelekea mama yangu kama ulivyosema, unajua Baba yangu alishatangulia mbele za haki, umetoa jogoo, siku ukienda Chato nitakukabidhi mama yangu na wewe uwe baba, asanteni sana watu wa Somanga." - Rais Magufuli.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger