7/16/2020

Rais Magufuli: Sijamtuma mtu kugombea ubunge na Hakuna Kiongozi yeyote Aliyemtuma Mtu YeyoteRais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi amesema kuwa hadi Julai 16, 2020 asubuhi zaidi ya wanachama 8,000 wa chama hicho walikuwa wametia nia ya kugombea ubunge.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni ambapo ameeleza Mkoa wa Dar es Salaam ndio unaongoza .

Aidha, Rais Magufuli ametumia wasaa huo kusisitiza kuwa taarifa kwamba baadhi ya watia nia wametumwa na viongozi wa serikali na chama akiwemo yeye na viongozi wengine wakiwemo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Makamu Mwenyekiti wa CCM au Katibu Mkuu wa CCM na viongozi wa vyombo vya ulinzi si za kweli.

Ametaka chama hicho kuwapima watia nia wote kwa usawa na kwamba wao hawajamtuma mtu, bali wanataka wananchi wachague wenyewe wa kumtuma.

Hata hivyo amesema uwepo wa idadi hiyo kubwa ya watia nia ni ishara ya kukomaa kwa demokrasia ndani ya chama hicho.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger