7/31/2020

Rapper Anayechukiwa na Kuitwa Snitch Tekashi 69 Kuachiwa Huru Rasmi Wikiendi hiiRapa machachari asiyeishiwa vituko kutoka pande za Brooklyn Marekani, Tekashi 69 anatarajia kuwa mtu huru kabisa, ambapo Leo Julai 30, anakua kabakiza siku tatu pekee kumalizia kifungo chake cha nje ambacho amekua akitumikia nyumbani kwake kwa muda wa miezi minne iliyopita.

Itakumbukwa, kwa karibu miaka miwili sasa rapa huyo amekua kifungoni kutokana na hukumu aliyoipata baada ya kupatikana na hatia ya makosa tisa ikiwemo kufanya malipo na umiliki wa silaha za moto makosa ambayo yangemfanya #Tekashi atumikie miaka 32 nyuma ya nondo, lakini Disemba 18, 2019, #Tekashi alipunguziwa hukumu na kufikia miezi 24 baada ya kutoa ushirikiano kwa serikali.

Muwakilishi kutoka upande wa 6ix9ine amethibitisha kuwa rapa huyo anatarajiwa kuachiliwa rasmi Jumapili hii Agosti 2.

Sanjali na hilo, mtandao wa Page Six umeripoti kuwa, kwasasa #Tekashi ataimarisha ulinzi wake zaidi pindi atakapokuwa huru uraiani.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger