7/29/2020

Serikali Yafafanua Ndege ya Kenya Kushindwa Kutua Tanzania


UBALOZI wa Tanzania nchini Kenya umekanusha taarifa kuwa ujumbe rasmi uliomwakilisha Rais Uhuru Kenyatta katika msiba wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ulizuiwa kutua nchini.

Ujumbe huo ulioongozwa na Samuel Losuron Poghisio ulilazimika kurejea jijini Nairobi kwa sababu ya hitilafu ya ndege ambapo serikali ya  Tanzania ilipewa taarifa.

Ubalozi umesema taarifa hizo za upotoshaji, uongo na zina lengo la kuzorotesha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya iliyotangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha Mkapa.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Uhuru Kenyatta alimwelezea  Mkapa kama shupavu aliyetetea maslahi ya Tanzania na Afrika kwa jumla

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger