Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Sheikh wa mkoa wa Dar Es Salaam: Makonda amelikoroga mwenyewe, siwezi kumpigia kampeni, ili iweje

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Sheikh mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Sheikh Alhadj Mussa Salum amekanusha taarifa kuwa aliwapigia Waislam wa Kigamboni kumchagua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kuwa Mbunge katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni.


Akiongea na Waandishi wa habari ameeleza kuwa kuna ujumbe ukiokuwa unatembea ukieleza kuwa yeye aliwapigia simu Waislam wote Kigamboni ili kumpigia kura Makonda.


“Mimi siwezi kufanya hivyo nilimsaidia na kumuombea wakati akiwa mkuu wa mkoa, sisi tunafanya hivyo tukijua anamsaidia Mh. Rais na sisi tunafanya kazi na kiongozi yetote, Makonda alilikoroga mwenyewe “


Mbali na hilo Sheikh wa Kigamboni pia amefafanua kuwa yeye akiwa kama kiongozi Kigamboni hakuna taarifa kama hizo.

Post a Comment

0 Comments