7/26/2020

Simba SC Yafuata Beki TP Mazembe


KLABU ya Simba imedhamiria kweli kusajili kikosi cha kimataifa baada ya kuwa katika mchakato wa kusajili beki matata kutoka katika Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.

Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hivyo imejihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao ambapo uongozi wa timu hiyo tayari umeshaweka wazi kutaka kufanya usajili kabambe wa wachezaji wa kimataifa ili kuleta ushindani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Championi Jumamosi, meneja wa mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere, Patrick Gakumba amefunguka kuwa, kuna mazungumzo kati yake na uongozi wa Simba juu ya kushusha beki matata kutoka TP Mazembe ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

“Nipo katika mazungumzo na viongozi wa Simba juu ya kuwaletea beki mwenye kiwango cha juu ambapo tayari nimeshampata beki huyo anayekipiga katika Klabu ya TP Mazembe japokuwa siwezi kumtaja kwa sasa ni nani kwa kuwa sheria inanikataza kumtaja mchezaji akiwa bado hajasaini.

“Mipango ikikamilika Simba watamsajili beki kutoka TP Mazembe ambaye ana uzoefu mzuri katika mashindano ya kimataifa kwani timu yake hiyo imeshawahi kufika fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Mazungumzo yanakwenda vizuri kati yangu na uongozi wa Simba na mambo yakikaa sawa basi nitamuweka wazi mchezaji huyo na dau watakalotumia kumsajili,” alisema Gakumba.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger