Tanasha Dona Atangaza Balaa Zito!MZAZI mwenza wa staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna ametangaza balaa zito.

Hivi karibuni Tanasha aliingia studio kwa prodyuza Shirko kule Mombasa ambapo amesema anatarajia kuiteka Afrika Mashariki kupitia projekti yake mpya aliyomshirikisha mtayarishaji huyo.

Kupitia Insta Story yake, Tanasha ameposti picha yake ya prodyuza Shirko wakiwa studio na kueleza kuwa muda si mrefu ataachia kitu cha hatari.

“Ni kolabo ya hatari. Ni T Donna na Shirko,” amesema Tanasha ambaye amezaa mtoto wa kiume na Diamond au Mondi aitwaye Naseeb Junior kabla ya kutengana mapema mwaka huu.

Shirko ni prodyuza mkongwe Bongo. Pia aliwahi kusikika kwenye ngoma kama Nataka Kuwa Nawe alioshirikiana na Berry White na Berry Black.

Shirko amehusika kwenye utengenezaji wa ngoma nyingi zilizotikisha za Yamoto Band na nyinginezo.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DAR

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments