7/16/2020

Top 5 Wachekeshaji Wa Kike Bongo WanaotikisaKILA tasnia ya burudani hapa Bongo, imekua ikitoa vipaji vikali ambavyo vinajizolea mashabiki lukuki kutokana na kile anachokifanya msanii husika.

 

Katika sehemu zote duniani zinazopenda burudani, kuna tasnia moja ambayo imekuwa ikizingatiwa na kufuatiliwa na watu wa rika zote; namaanisha watoto, na hata wazee, nayo ni uchekeshaji.

 

Hapa Bongo kumekuwa kukiibuka vipaji vikali sana vya uchekeshaji na kutoa burudani ya kutosha, kwani huwezi kuacha kuifuatilia.Makala haya yanakuletea Top Five ya wachekeshaji wa kike wanaofanya vizuri:

 

ASHA BOKO

Jina halisi ni Tatu Yusuph almaarufu Asha Boko, ni mmoja wa waigizaji wa kike wenye kuvunja mbavu.Kutokana na jinsi anavyotumia umbo lake kwenye sanaa ya uchekeshaji, imekuwa ikimfanya azidi kuongeza mashabiki kutokana na uigizaji wake.

 

Amedumu kwenye fani hiyo kwa zaidi ya miaka 10 tangu alipoanza kutamba na Kundi la Kaole Sanaa. Mbali na hilo, amecheza filamu kama Kizunguzungu, Shoe Shine, Street Girl, Boss, Teja, Karaha, Ngekewa, na nyingine nyingi.

 

TABU MTINGITA

Saimba Mtingita ndiyo jina la kwenye kitambulisho chake japo mshabiki wanamfahamu kama Tabu Mtingita.Tabu amekuwa akifanya maajabu sana katika tasnia hii ya uchekeshaji kupitia mitandao ambako anaposti clip za video zake.

 

Kupitia fani yake ya uchekeshaji, imemfanya apate dili la ubalozi katika kampuni ya maziwa ya Asas kutokea Iringa.Mbali na vichekesho vyake, pia ameonekana katika tamthiliya ya Kapuni ambayo inafanya poa kwa sasa.

 

EBITOKE

Ebitoke ni jina lake la sanaa japo wazazi wake walimpa jina la Anastazia Exavery.

Ebitoke ni msanii ambaye amekuza sana jina lake tangu akiwa na kampuni ya Timamu akiwa na wachekeshaji wengine kama Mkali Wenu, Bwana Mjeshi na Mr. Beneficial.

 

Amejizolea umaarufu kupitia uchekeshaji kiasi kwamba amejipatia madili mengi katika makampuni ikiwemo Kampuni ya Star Times na kwa sasa anamiliki channel yake ya Ebitoke Comedy katika mtandao wa YouTube.BLACK PASS

Ni muigizaji wa vichekesho kupitia mitandao ya kijamii ambaye amekuwa na kipaji cha kitofauti kutokana na uchekeshaji wake kwa kuvaa uhusika wa kiziwi.Ni mmoja kati ya wachekeshaji ambao wamekuwa wakifurahisha sana na kubadili uhusika pale inapombidi.

 

KATARINA WA KARATU

Jina halisi anafahamika kama Rosemary Urio almaarufu Katarina wa Karatu, amekuwa ni mchekeshaji ambaye anavunja mbavu anapokuwa mzigoni.Katarina amekuwa akifanya poa sana na aina yake ya uchekeshaji kwani mara nyingi amekuwa akitumia mitandao ya kijamii na majukwaani.

Mbali na kujizolea umaarufu, anakiri kuwa uchekeshaji umempa mafanikio makubwa katika kuendesha maisha yake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger