Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Trump Agoma Kuwalazimisha Wamarekani Kuvaa Barakoa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURELicha ya ongezeko la visa vya ugonjwa wa COVID-19, Rais Donald Trump amesema hakubaliani na kuwekwa amri ya wananchi kuvaa barakoa kwa kuwa anaamini watu wanapaswa kuwa na uhuru fulani.


Kauli yake inakuja baada ya Dkt. Anthony Fauci ambaye ni Mtaalamu wa Magonjwa ya Kuambukiza kusema ni muhimu kuvaa barakoa na kuwasisitiza viongozi wa miji kuhimiza wananchi kufanya hivyo.


Mapema wiki hii, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kilitoa tamko la kuwahamasisha wananchi wote kuvaa barakoa.


Tangu kuanza kwa mlipuko huo nchini Marekani, Rais Trump alionekana amevaa barakoa kwa mara ya kwanza Jumamosi iliyopita.


Mapema wiki hii, CDC ilitoa taarifa kutaka kila mtu avae barako.


Marekani imerekodi visa 3,719,494, vifo 140,733 na waliopona hadi sasa ni 1,688,243

Post a Comment

0 Comments