Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Tundu Lissu Atoa Mpya "Wale Waliokuja Kuniua Bado Wanaitwa Wasiojulikana"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Makamau mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleoa (Chadema), Tundu Lissu amesema waliotaka kumuua hadi sasa wanaitwa wasiojulikana maana yake bado wapo na hawajasema kama lengo lao wameliacha.

“Bado kuna hatari ya maisha yangu ninarudi nchini katika mazingira ya hatari dhidi yangu haijaondoka lakini narudi tu ni nyumbani kwetu,” amesema Lissu.

aliongezea kuwa “Ninafahamu kwamba mamilioni yenu mlilia, mliomba Mungu na kujitolea hapa nilipo nina damu ya Watanzania nisiowajua, nina damu ya wakenya nisiowajua kwa sababu niliwekewa damu mara tatu ya ujazo wangu wa kawaida katika hospitalia ya Nairobi,”.

Aidha, Lissu amesema ataingia nchini Jumatatu ya Julai 27, 2020 majira ya saa 7:20 mchana  akiwa kwenye ndege ya Shirika la Ethiopia.

“Kwa kipindi hiki nina mambo mengi sana yaliyo kichwani mwangu ambayo ni vigumu kuyaeleza yote naomba nisema tu wale waliotumwa kuja kuniua na waliowatuma hawakutegemea kwamba siku kama ya leo nitakuwepo na nitakuwa nazungumza nyumbani,” amesema Lissu.

Post a Comment

0 Comments