7/14/2020

"Ukiachwa Usipingane na Ukweli" - Miriam Mauki


Mtaalamu wa masuala ya malezi na mahusiano, Miriam Mauki amesema kuwa mtu yeyote ambaye ataachana na mpenzi wake, hatakiwi kuendekeza hasira badala yake asamehe na kuamua kuendelea na maisha yake na akubaliane na ile hali ya kwamba ameachwa.

Miriam ameitoa kauli hiyo siku za hivi karibuni, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio na kuongeza kuwa mtu anapoamua kuendekeza hasira zake inamfanya kutomsahau mpenzi wake wa awali na kubaki na majuto na machukizo moyoni mwake.

"Kama umeachwa usiendekeze hasira na usipingane na ukweli wa kwamba ameakuacha na hakuna haja ya kujiua, na usikimbilie kwenye mahusiano mengine, tujifunze mazuri usitangulize ubaya na ukumbuke yale mema mliyowahi kufanya pamoja, samehe ondoa hasira na jifunze kuishi bila huyo mtu"  amesema Miriam Mauki.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger