7/30/2020

Unaambiwa India Yanunua Ndege Moja Hatari Sana Inaitwa ‘RAFALE’ , Inauwezo wa Kushambulia Angani na Ardhini Bila Kukosea


Jeshi la India limepokea ndege tano za kivita aina ya Rafale huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kati yake na China. Ndege hizo ni miongoni mwa makubaliano ya taifa hilo na lile la Ufaransa yaliofanyika mwaka 2016 kununua ndege 36.

Delhi inatumai kuimarisha jeshi lake la angani linalotumia ndege za zamani za kisoviet kupitia nununuzi wa ndege hizo mpya. Lakini watalaamu wanaonya kwamba ndege hizi haziwezi kutumika moja kwa moja iwapo kutakuwa na vita.

Mwanaanga mstaafu Pranab Barbora, ambaye alisimamia ununuzi wa ndege za kivita aina ya jaguar aliambia BBC kwamba kuwasili kwa Rafale ni hatua nzuri kwasasabu itaimarisha uwezo wa jeshi la angani.

”Lakini itachukua muda kabla ya ndege hizi kuanza kufanya kazi . Lazima uweke msururu wa kimkakati, kuwafunza mafundi na wafanyakazi wa ardini nchini India”, alisema.

Aliongezea kwamba inachukua hadi miaka miwili kabla ya kikosi kipya kuanza operesheni.

Kikosi hicho cha Rafale kitaanza kufanya kazi kitakapomiliki takriban ndege 18. Kuwasili kwa ndege nyengine kunatarajiwa kukamilika mwaka ujao.

Ndege hizo zilizotengenezwa na kampuni ya Ufaransa ya Dassault Aviation, ziliondoka nchini Ufaransa siku ya Jumatatu na kuwasili UAE ambapo zilitua kwa muda kabla ya kuondoka na kuelekea India.

Safari hiyo ilionyesha uwezo wa ndege hizo pamoja na uwezo wa kujazwa mafuta zikiwa angani.

Ndege aina ya Rafale ni ndege ilio na uwezo wa kufanya vitu tofauti ikiwemo kusafiri umbali mkubwa ikiwemo kufanya mashambulizi ya angani na ardhini bila kukosa.

Wachambuzi wanasema kwamba kuwasili kwa ndege hiyo kutapiga jeki motisha ya jeshi la angani ambalo limekuwa likikabiliwa na upungufu wa ndege za kijeshi.Members of the Air Force contingent pose with a mockup of the Indian Air Force tableaux for the Republic Day Parade featuring the Rafale fighter jet.

Ndege Rafale itaimarisha jeshi la anga la India
India inahitaji ndege 42 iwapo itakabiliwa na vita dhidi ya China na Pakistan.

Lakini kikosi chake cha wanahewa kimepunguzwa hadi 31 kutokana na kuzeeka kwa ndege za zake zilizotengenezwa nchini Urusi.

Ununuzi wa ndege hizo za kijeshi umekuwepo kwa miaka kadhaa sasa.

Chama tawala cha BJP kilianza mchakato huo mwaka 2000 na mrithi wake utawala uliongozwa na chama cha Congress, uliendeleza azma hiyo na kutoa zabuni 2008 kununua ndege 126 za kivita.

Kampuni ya Dassault ilipatiwa zabuni hiyo 2012, na kampuni ya serikali ya Hindustan Aeronautics Limited HAL lilichaguliwa kama mshirika wa kutengeneza ndege 108 nchini India.

Wakati BJP kiliporudi madarakani chini ya uongozi wa Narendra Modi 2014, ununuzi wa ndege hizo ulipatiwa kipau mbele.

Lakini badala ya kupeleka makubaliano hayo mbele, aliwashangaza wengi kwa kuagiza ndege 36 za kivita ikiwa ni miongoni mwa makubaliano mapya ambapo HAL haikushirikishwa.

Serikali ya India inasema kwamba iliamua kununua ndege 36 za kijeshi kwa haraka ili kuangazia upungufu wa jeshi lake la angani.

Lakini haijulikani ni wapi India itazinunua ndege zilizosalia inazozihitaji katika siku za usoni.

Jeshi la angani lilitangaza 2018 kwamba itawasilisha zabuni za takriban ndege 110 za kivita lakini mkataba huo haujakamilishwa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger