Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Uongozi wa Yanga "Hatujui Bernard Morrison Anaishi Wapi ila Tunamlipia Kodi, Kazidisha Utovu wa Nidhamu"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Patrick Simon amesema mchezaji wao Bernard Morrison amepelekwa kwenye kamati ya maadili kutokana na matukio yake ya utovu wa nidhamu kujirudiarudia.

“Kwanza nimeshachoka sana habari za Morrison lakini ni kwamba kuna kamati ya maadili ya Yanga inashughulikia suala lake muda si mrefu watalitolea maamuzi kwa sababu baada kuwa yametokea matendo ya kujirudia kila siku ilibidi tumpeleke kwenye kamati ya maadili ambayo ni huru ambayo mimi sipo kwenye hiyo kamati.”

“Kwa hiyo wanafanya taratibu zao wameshamwalika kumsikiliza na kufanya taratibu zao halafu watatoa uamuzi wao, sisi tunawasubiri wao pamoja na TFF watuambie maamuzi yao juu ya kesi yake.”
“Tuna kamati ya maadili ambayo inafanya maamuzi juu ya kilakitu kuhusu masuala ya Morrison kuivuruga klabu. Tunachokitaka sisi Yanga tupate suluhisho la kudumu kuhusu Morrison.”

KUVAA JEZI YA YANGA KWENYE MECHI ZA MITAANI.

“Hata akivaa jezi ya klabu huko mtaani sisi hatuna tatizo kwa sababu kuna mashabiki wengi huko wanavaa mitaani kwa hiyo kwetu sio tatizo. Sisi tunatafuta suluhisho la kudumu ambalo litapatikana muda si mrefu.”

MORRISON ANAISHI WAPI?

“Kusema kweli Morrison hatukuwa tumempa makazi ila tulimwambia atafute nyumba sisi tutalipia kwa hiyo nikisema amehama makazi nitakuwa nadanganya kwa watanzania. Sisi tunamlipia kodi na mpaka sasa hivi tunafanya hivyo.”

Post a Comment

0 Comments