Vijana CUF Wamtaka Prof Lipumba Kuwania Urais, Wamchukulia Fomu na Kumkabidhi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Vijana wa Chama Cha Wananchi CUF Mkoa wa Dar es Salaam hii Leo wamesema Wana Imani katika wagombea wote wa upinzani ambao wamepitishwa na vyama vyao kuwania nafasi ya Urais


Vijana wa Chama Cha Wananchi CUF Mkoa wa Dar es Salaam hii Leo wamesema Wana Imani katika wagombea wote wa upinzani ambao wamepitishwa na vyama vyao kuwania nafasi ya Urais hawamuwezi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM isipokuwa Mwenyekiti wa Chama Hicho Taifa Prof Ibrahim Haruna Lipumba.

Mapema asubuhi hii leo vijana hao wamejitokeza katika ofisi ya Wilaya ya Chama Hicho kinondoni ambako anaishi Mwenyekiti wao ambapo kwa kujichangisha wenyewe wameamua kumchukulia fomu na kumkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo Mkiti wa chama hicho Taifa prof Lipumba amesema aliamua kukaa kimya ili kutoa nafasi kwa wanachama wengine wajitokeze kuchukua Fomu ili kupambana ambapo amesema yapo mengi ambayo kama Chama wanaamini bado ni matakwa ya wananchi na hayajatekelezwa na serikali.akiahidi endapo atapata ridhaa Basi ataunga serikali ya Umoja wa kitaifa ikiwemo kukamilisha mchakato wa katiba mpya.

Kwa mujibu wa chama hicho kesho Tarehe 24 July ndiyo siku ya mwisho ya kurejesha fomu ya wagombea kwa ngazi ya Urais hivyo atalazimika kuijaza fomu hiyo kwa kuwa vijana wa Chama Cha CUF wameonesha Imani kubwa Kwake kuwa anaweza kuwavusha.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad