Viongozi wa Chadema Wapigwa Marufuku Kuwapokea Walioshindwa CCM Kwenye Kura za Maoni

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa wa Njombe kimewaagiza viongozi wa Majimbo na kata zote za mkoa huo kuto kumpokea mwanachama yeyote aliyeshughulikiwa kwenye kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi. 


Agizo hilo limetolewa na mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Njombe Rose Mayemba,huku akidai kupata taarifa za baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwenye maeneo kadhaa ya mkoa wa Njombe wakianza kuonyesha nia ya kujiunga na Chama hicho kwa lengo la kutafuta nafasi tena mara baada ya kushughulikiwa kwenye Chama chao. 


"Nimepata taarifa kuwa kuna wagombea Udiwani wa CCM walioshughulikiwa kwenye kura za maoni wanataka kuja kugombea CHADEMA,hiyo nafasi haipo"alisema Rose Mayemba 


Rose amewataka viongozi wa Chama hicho kuto kuwapokea wanaChama hao. 


"Tafadhali nawaagiza viongozi wangu kwenye Majimbo na kata zote 107 za mkoa wa Njombe msiwapokee (walioshughulikiwa) hawa ni wale walionzisha biashara haramu ya nunua nunua ya viongozi kwa kisingizio cha kuunga juhudi"alisema tena Rose Mayemba 


Vile vile Rose ametoa wito kwa wanachama hao kubaki kwenye vyama vyao na waendelee kuunga juhudi wakiwa wanaChama wa kawaida sio lazima wawe na vyeo ndo waunge Juhudi. 


Aidha amesema 


"Sisi kwenye kila kata kuna wagombea kuja kwao ni kutaka kuleta vurugu kwenye Chama,wabaki huko waliko wajitafakari upya ama wakubali tuwapokee kama wanachama wa kawaida na watusaidie kuwatafutia kura wagombea watakaopitishwa na chama" aliongeza Rose Mayemba 


Taarifa ya mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe imekuja ikiwa imepita siku moja tangu kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi huku mchakato ukiwa umekamilika kwa kuwapata wagombea wa Udiwani wa Viti maalum kupitia jumuiya ya umoja wa wanawake UWT,madiwani wa Kata pamoja na Ubunge huku Chama hicho kikitarajia kuingia katika hatua nyingine ya mchakato ikiwemo vikao vya kamati kuu ngazi za wilaya,Mikoa na Taifa.Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad