7/15/2020

Walioshinda Kura za Maoni za Ubunge Chadema


WASHINDI  wa uchaguzi kwenye kura za maoni za ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) waliopita kwenye majimbo yao ni kama ifuatavyo:1.Mshindi Jimbo la Kawe ni Halima Mdee mwenye kura 63 (71.5%).

2. Tarime Mjini mshindi ni Esther Matiko mwenye kura 80 (97. 6%).

3. Tarime Vijijini mshindi ni John Heche ambaye amepata kura 268 (99.2%).

Heche alikuwa mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndiyo au Hapana, kwenye kura zilizopigwa, kura za Ndiyo ni 268 (99.2%), zilizoharibika ni 2 (0.74%) hapakuwa na kura ya Hapana

4. Mshindi Jimbo la Bunda Mjini ni Ester Bulaya  kura 126

5. Jimbo la Iramba mshindi ni Jesca Kishoa  kura 134 (98%).

Jesca alikuwa mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndiyo au Hapana, kwenye kura 136 zilizopigwa, kura za Ndiyo ni 134 (98%), zilizoharibika ni 2 na hakuna kura ya Hapana.

6. Jimbo la Isimani mshindi ni Patrick Ole Sosopi mwenye kura 115 (82.6%).

7. Mshindi jimbo la Mbeya Mjini ni Joseph Mbilinyi (Sugu) mwenye kura 294

– Sugu alikuwa ni mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndiyo au Hapana ambapo amepata Ndiyo 294 na Hapana 5.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger