7/14/2020

Wasanii Kutumika Kisiasa Badala ya Kuunganisha Watu...Yupo Wapi Marlaw Aliyetumika Kisiasa Mwaka 2010

Mwaka 2015, Diamond Platnumz, alipanda jukwaani Arusha, Sheikh Amri Abed Stadium, kutumbuiza wakati Edward Lowassa alipotangaza nia ya kugombea urais. Kisha, wakati wa kampeni alimpigia debe Rais John Magufuli aliyekuwa anapambana na Lowassa. Ni fedha tu.

Wasanii wa Tanzania walitia fora mwaka 2015. Walipanda jukwaani kuwapigia kura wagombea waliokuwa wanashindana na wasanii wenzao. Ilitokea Mikumi kwa Profesa Jay, vilevile Mbeya Mjini kwa Sugu.

Mwaka 2015, wasanii kama Juma Nature, Ray Kigosi, Aunty Ezekiel na wengine, walipewa hela wakawa upande wa Lowassa, yaani Chadema na Ukawa. Badaye wakapandiwa dau, wakageukia kwa Magufuli, kwa maana ya CCM. Ni kwa sababu wasanii wetu hawana misingi. Uoga na fedha ndivyo vinaendesha akili zao. Wanavyoishi utadhani ni wasanii wasio na sababu yoyote katika sanaa wanayoitumikia.

Mwaka huu, wasanii wanapaswa kujiheshimu. Wasipelekeshwe na fedha wala hofu. Wanatakiwa kutumia sanaa zao kuwaunganisha watu. Wasanii kutumika kisiasa ni matokeo ya kuwa na sanaa bila misingi. Na sanaa bila misingi ni janga.

Yupo wapi Marlaw ambaye aliigeuza hit song yake ya Pii Pii (Missing My Baby) kuwa wimbo wa kampeni Uchaguzi Mkuu 2010. Baada ya hapo alipotea mazima. Sasa hivi wasanii kila mtu yupo bize kuandika nyimbo za kampeni. Wajitazame sana. Wanazingua bigtime na hivyo vinyimbo vyao vya kampeni. Vinyimbo vya kujikomba.

Unajua nini? Wasanii wa Bongo huu ni muda wa kutumika. Watasimama majukwaani kukata mauno, kupiga kelele kwenye majukwaa ya wanasiasa, watawakwaza mashabiki wao, watapewa pesa na kuona maisha wameyapatia. Baada ya uchaguzi watatelekezwa. Shida zao zitabaki palepale.

Mwaka 2025 ukiwadia, watatumika tena kwenye kampeni na watachekelea. Wataona maisha ni poa. Watatunga na kuimba nyimbo nyingine. Shida zao zitakuwa ni zilezile zinazowafanya wabaki maskini hadi kutegemea kampeni za uchaguzi.

Wasanii Bongo wapo kama wapiga kura enzi za ujima, baada ya uchaguzi, wanatelekezwa. Hawakumbukwi. Changamoto zao hazitatuliwi. Wanabaki maskini. Uchaguzi mwingine ukifika, wanapewa ‘vijihela’, fulana na kofia, au hata chakula. Kisha wanasahau.

Ndimi Luqman MALOTO
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger