7/18/2020

Wasanuii wa Kike Wenye Pesa Ndefu Bongo


KWA wasanii wa kiume, Nasibu Abdul ‘Dimaond Platnumz’ ndiye anayetajwa kuongoza kwa kuwa na mkwanja mrefu zaidi lakini hata hivyo, kwa upande wa wasanii wa kike, wapo wanaotajwa kuwa na mkwanja mrefu pia!

Makala haya yanakuletea wasanii wa kike matata hapa nyumbani ambao wanatajwa kuwa na mkwanja wa kutosha:

VANESSA MDEE

Vanessa Mdee ni mwanadada kutoka mkoani Kilimanjaro kama jina la mkoa wao “Moshi” inavyotafsiriwa na watoto wa kule kuwa kirefu chake ni “Mungu Onyesha Sehemu Hela Ilipo”, Vanessa ameweza kuutendea haki usemi huu.

Mwadada huyu japo kaamua kukimbia gemu la muziki, lakini ndiye msanii anayetajwa kuwa wa kwanza mwenye mkwanja mrefu kati ya wasanii wote wa kike hapa Bongo,na hii ni baada ya kupata dili la Afrika Got Tallent. Akiwa kama Judge,Pia ameweza kupata shoo kubwa Nchini Marekani iliyolipwa Dola elfu 40 kwenye  kupafomu.

LADY JAY DEE

Judith Wambura ndiyo jina halisi alilobatizwa, lakini jina la kutafutia pesa anapenda kujiiita ‘Lady Jay Dee’au Komando. Ni mwanamuziki kingongwe hapa Bongo na bado anafanya poa katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ya “Wife” aliyefanya na Harmonize, mwanamama huyu amepata umaarufu mkubwa kutokana na staili ya uimbaji wake.

Pia amefanya mambo makubwa ikiwemo kupeperusha bendera ya Tanzania, kwa kufikisha muziki wa Bongo Fleva hapa ulipofika, Mwanamama huyu inasemekana ana utajiri wa Billioni 9.2.

NANDY

Kiboko wa “Acha Lizame” Faustina Charles Mfinanga ”Nandy” huyu ni msanii ambaye amepata mashavu makubwa na mengi, kama vile DSTV,SABUNI na mengine mengi lakini kubwa zaidi katika zote ni  Nandy Fetival iliyomuingizia zaidi ya Dola za Kimarekani elfu 80, pia V.I.P Show ya Nchini France aliyolipwa zaidi ya Dola 38 kupafomu.

Mwanadada huyu amefanya shoo nyingi sana zilizompa pesa na kumfanya mwanadada Nandy kuingia kwenye wasanii wa kike wenye mkwanja mrefu hapa Bongo.

WEMA

Ukiambiwa utaje wasichana wanaofanya vizuri katika gemu ya filamu nchini, basi naamini hautasita kutaja jina la mwanadada mrembo na mwenye mvuto wa aina yake Wema Issac Sepetu, ambaye umaarufu wake ulionekana zaidi mwaka 2006 mara baada yakunyakua taji la Miss Tanzania.

Ukiambiwa Umaarufu wake ulizidi kuonekana zaidi pale alipoingia katika fani ya uigizaji na kufanikiwa kucheza muvi ya A point of no return aliyoshirikiana na marehemu Steven Charles Kanumba, sauti yake ya kitoto akiongea na jinsi anavyovaa uhusika pindi anapokuwa mbele ya camera ndio vitu vinavyomfanya mrembo huyo azidi kuwa juu.

Twiga ndivyo anavyojiita sasa,  ameingia kwenye chati ya wasanii wa kike wenye pesa chafu, hii ni kutoakana na speed aliyokuwa nayo mwanamke huyu ya kusaka pes ilipojificha, na wengi wanasema kwa mwendo aliokuwa nao sepetu anaweza hata akamfikia Nandy.

Kwa sasa hivi anayo App yake  inayojulikana kwa jina la Cokie  with wema Depetu, ambayo huwa anafanya na mastaa wa hapa Bongo .kinayoweza kudownlodiwa na mamilioni ya watu ndani na hata nje ya Bongo, pamoja na madili mengine aliyokuwa nayo ya Ubalozi wa makampuni mbalimbali.

WOLPER

Mama anayependa Dogo Dogo, Ni mwigizaji wa filamu za  Bongo Jaqcline Wolper amepata umaarufu mkubwa toka enzi za marehemu Kanumba , huyu amejipatia pesa zaidi, kulingana na ubunifu wake wa mavazi, inayojulikana kama “Wolper Stylish”,

Mavazi yake ni Unique  na watu wametokea kuyapenda zaidi, na kujikuta akipata madili makubwa ya kuwavalisha watu wenye wazifa kwenye nchi mbalimbali.

Lakini pia Wolper amewavisha wake wa Marais Tanzania na Kenya ambayo ilimpa fedha kubwa, amepata pesa kulingana na upambanaji wake wa kibiashara ,kwa sababu amekuwa anatumia muda mwingi kwenye biashara kuliko hata kuigiza muvi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger