7/16/2020

Wassira Awajia Juu Wanaosambaza Picha yake Aliyosinzia Bungeni


Mwanasiasa Mkongwe wa Tanzania Mzee Steven Wasira ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 75 amewajibu Watu wanaoisambaza picha yake anayoonekana kasinzia Bungeni, amesema anaamini kuna baadhi ya Watu wameirudisha picha hiyo ya zamani sasa kutaka kumchafulia.

Mzee Wasira anaamini Watu hao wamefanya hivyo sasa hivi baada ya yeye kutangaza nia ya kutaka kugombea Ubunge Jimbo la Bunda kwenye uchaguzi mkuu wa October mwaka huu ambapo amesema “ile siku ya hii picha nilikua na mafua”“Nilikua na mafua nikanywa dawa ya mafua siku moja katika maisha yangu ikapigwa picha siku hiyo, ile picha haiwezi kuakisi maisha yangu, mbona niko Halmashauri kuu ya Taifa hawajapiga nyingine?” – Wasira

“Huo ni ujinga Watu na propaganda zao wanataka kutumia mitandao ya kijamii vibaya” amemalizia kwa kusema hayo Mzee Steven Wassira.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger