7/23/2020

Watumishi Tisa wa Takukuru Wamesemamishwa Kazi Sakata la MagufuliMkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bregedia Jenerali, John Mbung’o amewasimamisha kazi watumishi tisa.

Watumishi hao ambao wamesimamishwa kazi wamehusika katika ujenzi na usimamizi wa majengo saba ya Takukuru.

Majengo hayo ambazo yapo Chamwino, Mpwapwa, Ngorongoro, Manyoni, Masasi, Namtumbo na Ruangwa.

Mbung’o amesema imeundwa Tume yenye watu wanne kutoka nje ya Takukuru kwa ajili ya kufautailia kama kuna ubadhirifu uliofanyika katika majengo yaliyojengwa.

Jana Rais John Magufuli, wakati akizindua jengo la Chamwino alisema anayazindua huku moyo wake ukimuua kwa kuwa Takukuru wamepigwa katika ujenzi huo.

Magufuli amesema jengo kama hilo halina uhalisia wa thani ya Sh milioni 134 kwa kuwa yeye alishwahi kujenga nyumba ya aina hiyo kwa Sh milioni 40.

Rais aliagiza kufanyika kwa uchunguzi wa ujenzi wa nyumba hizo kutokana na gharama zake kuwa kubwa huku akiwashaanga Takukuru iweje na wao wapigwe fedha katika nyumba hizo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger