7/31/2020

Waziri Mkuu ampa neno Sheikh Majini


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewashukuru viongozi wa Dini ya Kiislamu, waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao, huku akimpa moyo Shekh Majini kwamba huenda akapitishwa kugombea nafasi ya Ubunge.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 31, 2020, wakati wa Swala ya Eid-El-Adhaa, ambayo Kitaifa imefanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, na kuwaambia kuwa wameonesha njia kwa jamii kwamba kuomba nafasi ya uongozi Serikali si ya watu kadhaa bali hata viongozi wa Dini wanaweza kufanya hivyo.

"Mwaka huu nimefurahi nimeona hata viongozi wa Kiislamu mmejitokeza kwa wingi kugombea, Sheikh Majini mchakato unaendelea tunakuombea sana, kile kikao cha mwisho kikurudishe, lakini wajumbe wale wametoa mwongozo tu maamuzi yako juu huko, tunaamini InshaAllah kule Handeni utakuwa Mbunge", amesema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu akatoa msisitizo kuhusu suala la Uchaguzi ulio huru na wenye haki, "Lazima tuhakikishe zoezi la uchaguzi mwaka huu linaenda kwa amani na utulivu, sisi Serikali kiongozi wetu wa nchi ametuhakikishia kwamba uchaguzi mwaka huu utakuwa wa huru na haki, tuende na hilo tusianze kujengeana mashaka na inawezekana".
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger