7/28/2020

Wema awaka kisa mtoto "Usipende kuzungumza kitu kinachoniuma "Miss Tanzania mwaka 2006, Mwanadada Wema Sepetu ameonyesha kuchukizwa na wale wanaotonesha kidonda chake cha kutopata mtoto kwenye mitandao ya kijamii. 


Wema ameeleza hayo mara baada ya shabiki mmoja kumgusia suala hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram. 


“Sina jinsi mpenzi wangu, na sitokuwa mwanamke wa kwanza aliyekosa mtoto na hata hivyo naridhika tu na kitendo cha kuwapenda watoto hata kama sina one to call my own,” amesema. 


“Yote ni mipango ya Allah, mimi ni mja wake wake tu, ila sio kwamba sitaki, namtamani sana, but kama sio maajaliwa yangu basi. Alhamdulilah for everything. Usipende kuzungumza kitu kinachoniuma ukajifanya you know well, sijapenda,” amesema. 


Aidha, Februari mwaka huu kupitia WemaApp, mrembo huyo alisema amekaribia kakata tamaa ya kupata mtoto baada ya kudai anaamini anaandamwa na laana ya kutoa mimba mbili za mwigizaji Steven Kanumba ambaye kwa sasa ni marehemu. 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger