7/31/2020

“Wewe umeharibu barabara, nakushughulikia ngoja nifike DAR” Rais Magufuli atoa onyo (+video)


Rais Dkt. John Magufuli akiwa njiani kurudi DSM ametoa maagizo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelewe kuhakikisha barabara ya Lindi inajengwa katika maeneo yote yaliyoharibika.

”Mmeniudhi Wizara ya Ujenzi, sijafurahia. Nimetoka na machungu kwa kumzika Mzee Mkapa, lakini hapa Somanga napo nimepata machungu kwa kukuta barabara hii haijatengenezwa” Rais Magufuli

“Barabara hii ya Mtwara-Lindi-DSM imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange, utunzaji sio mzuri” Rais Magufuli

“Hii barabara imeharibika, huwezi ukaamini kama tuna Waziri wa Ujenzi. Kilometa 90 zote nilikuwa nahesabu zimeharibika” Rais Magufuli


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger