Yanga SC Inatia Huruma, Wachezaji 8 Out

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



YANGA inayonolewa na Kocha Mkuu, Luc Eymael, kesho inashuka uwanjani kumenyana na Lipuli FC kwenye mchezo mwisho wa Ligi Kuu Bara bila kuwa na nyota wake nane jambo ambalo linamliza kocha huyo.

Nyota hao wa kikosi cha kwanza ni pamoja na Lamine Moro ambaye anasumbuliwa na majeraha aliumia kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Mapinduzi Balama, Haruna Niyonzima, Papy Tshishimbi hawa wote ni majeruhi.

Mshambuliaji Patrick Sibomanayeye ana matatizo ya kifamilia, beki kisiki Kelvin Yondani hajaripoti kambini, Deus Kaseke yeye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliipata kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Bernard Morrison kiungo ambaye yupo kwenye mgogoro na Yanga kuhusu mkataba wake.

Eymael ameliambia Championi Jumamosikuwa, ni wakati mgumu ambao anapitia kwa sasa kwa kuwa anaingia vitani bila kuwa na silaha za kazi zile ambazo anazitegemea.

“Nipo kwenye wakati mgumu kwa sasa, ninamaliza mchezo wa mwisho na malengo yakiwa ni kumaliza tukiwa nafasi ya pili naona mambo magumu, sina Lamine, Kaseke ambaye ana kadi, Tshishimbi, Haruna, Balama hawa wote ni majeruhi.

Yondani hata sijui yupo wapi, Morrison najua tabia yake inajulikana, sijui itakuaje?” alisema.Lipuli inapambana kusaka nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 44 haina uhakika wa kubaki ikiwa itapoteza huku Yanga ipo nafasi ya tatu inapambania nafasi ya pili ikiwa na pointi 69 sawa na Azam FC iliyo nafasi ya pili wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa zote zimecheza mechi 37.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad