Yondani Atoweka Yanga, Kocha Amtafuta


BEKI wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani hajaonekana kwenye timu hiyo tangu baada ya kutoka sare dhidi ya Mwadui katika mchezo Ligi Kuu Tanzania Bara.

Inaelezwa baada ya mchezo huo ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1, huku beki huyo akiwa ni mmoja kati ya wachezaji waliocheza, amepotea bila kuwepo kwa taarifa katika benchi la ufundi.

Akizungumza na Championi Jumatano,kocha mkuu wa timu hiyo, Luc Eymael baada ya kuwasili mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wao leo Jumatano dhidi ya Mtibwa, amesema hajui mchezaji huyo alipo tangu walipomaliza mchezo wa Jumamosi.

“Kiukweli sijui yupo wapi na hadi sasa hakuna nilichoelezwa kwa sababu baada ya mechi Jumamosi, hakuja mazoezini, nilimuuliza meneja akaniambia hajui yupo wapi na hakuwa na taarifa naye.

“Lakini hata siku iliyofuata hakuja na hakukuwa na majibu yoyote kutoka kwa meneja kitu ambacho kimenikera, wanamuachaje mchezaji afanye mambo anayotaka tukiwa bado tuna mechi mbili muhimu za ugenini,” alisema Eymael.

Yondani ni kati ya wachezaji wazoefu na muhimu sana kwenye kikosi cha Yanga ambacho kwa sasa kinahaha kuhakikisha kinamaliza ligi katika nafasi ya pili.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments