Albamu Mpya ya Burna Boy ni moto mkali sana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Saa hizi niko mtandaoni nasikiliza Album ya Burna Boy ya "Twice As Tall" na nimefurahishwa nayo kupita kiasi.Niseme tu, nadhani huyu jamaa ana kipaji kikubwa na kila siku anazidi kukomaa tu. Humu ndani wametokea wasanii wakubwa duniani kama Youssou N'Dour, Christ Martin (Vocalist wa Cold-Play) na Naughty By Nature.

Kuimba na wasanii wakubwa kama hawa na kwenda nao vizuri kwa mahadhi ya kiafrika siyo kazi rahisi. Nilidhani album yake ya African Giant ndiyo kazi yake bora sana ya muda wote, lakini hii Twice As Tall ni nzuri zaidi. Naamini wasanii wetu wana kitu kikubwa cha kujifunza kutoka kwa Burna Boy.

Nilikuwa najiuliza kwanini wasanii wenye uwezo mkubwa kama Sauti Sol hawatambuliwi kama inavyotakiwa hapa Afrika Mashariki, lakini naamini baada ya hii Album kutoka Sauti Sol watapata kutambulika kimataifa na kupata heshima wanayoistahili. Msanii mkubwa kama Burna Boy kuwashirikisha Sauti Sol kwenye Album kubwa hivi inaashiria kwamba ameukubali uwezo wao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad