8/06/2020

"Alikiba Naomba Usinifokee Kabisa" -Mbwana SamattaMtanzania na mchezaji wa kimataifa wa Klabu ya Aston Villa Mbwana Samatta amemtaka msanii Alikiba asimfoke na kumtambia kuelekea kwenye mchezo wa SamaKiba utakaochezwa siku ya August 8 uwanja wa Benjamin William Mkapa.


Mbwana Samatta amesema amejipanga kwa ushindi kwa mara ya tatu mfululizo na mapato yatakayopatikana katika mchezo huo utapelekwa kwenye Wizara ya Elimu ili kushughulikia changamoyo ya masuala ya elimu hapa nchini.

"Timu yangu ya ushindi kama kawaida nimejiandaa kushinda kama michezo miwili iliyopita, naona figisu za marefa zimeanza lakini nina uhakika nitashinda tena kwa mara ya tatu mfululizo kwa sababu sijaona kizuizi, mimi nimemaliza maana Alikiba kaongea saa 2, Haji Manara naye kaongea saa 4, na Alikiba usinifokee kabisa nitakuchapa hata ufanye nini" amesema Mbwana Samatta 

Team Samatta amegusia timu yake itakuwa na wachezaji kama Kagere na Yondani na msemaji wake ni Haji Manara, huku Team Kiba itakuwa na wachezaji kama Ibrahim Ajib, Abdu Kiba na msemaji wake ni Official Mwalubadu.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger