8/04/2020

Aliyemtusi Rais JPM Facebook Ahukumiwa Jela Miaka Mitatu


KIJANA aliyemtukana Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt John Magufuli katika mtandao wa Facebook amehukumiwa kulipa faini ya shillingi millioni 5 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukutwa na hatia hio.

Kijana huyo anaetambulika kwa jina la Fadhili Silwimba, ni mkazi wa kijiji cha Nzoka Wilayani Momba Mkoani Songwe.

Hakimu Mkazi Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe, Kassim Mkwawa, amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 23(I) na (II) cha mwenendo wa makosa ya kimtandao namba 4 ya mwaka 2015.

Awali mwendesha mashtaka wa Serikali, Flavian Leonard Chacha, alisema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo, mnamo Septemba 7, 2019, kwa kutuma ujumbe wa kumtusi Rais kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger