8/03/2020

Aliyepona Ukimwi Bongo Aibuka na Mpya!ARUSHA: MWANAMKE Rose Lyimu, mkazi wa Arusha aliyeibuka hivi karibuni na kudai kuwa amepona ugonjwa wa Ukimwi (VVU), alioishi nao kwa zaidi ya miaka 12, ameibuka na mapya juu ya ugonjwa huo.Akizungumza Jumatano wiki hii na mwandishi wetu, Rose amesema ukombozi kwa wenye tatizo hilo upo kwenye tiba asili.

“Sijui kwa nini tunapuuza tiba hizi, mimi zimenifufua, maana nilikuwa nimekufa.

“Niliugua nikabaki na CD4 mbili (seli nyeupe za damu zinazohusika na kinga ya mwili), nikapukutika mwili hadi kufi kia kuwa na kilo 22.“Nililazwa hospitali moja jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu, nimetumia vidonge vya kufubaza virusi ‘ARVs’, lakini haikuwezekana kujinusuru na makali ya ugonjwa huu.“Ikabidi ndugu zangu wanirudishe nyumbani Arusha, siyo kuja kujiuguza tena, bali kusubiri kufa.

“Kwa kiasi kikubwa nilitengwa na jamii, nilinyanyapaliwa na kusema kweli nilikuwa mnyonge mbele ya watu na hata ndugu zangu.

“Nilipofi ka huku, nikaanza kutumia dawa za asili, kwa muda mfupi nikaona hali inabadilika, nikaanza kupata nguvu.“Nilipokwenda hospitali, madaktari walinishangaa, CD4 zilipanda katika hali ya kushangaza na mwisho wa siku nilipopimwa nikakutwa sina virusi vya Ukimwi, namshukuru Mungu,” alisema Rose.Aliongeza kuwa, alipata maambukizi ya ugonjwa huo mwaka 1999 ambapo mpaka takwimu za dunia zinachukuliwa mtandaoni na mwandishi wetu, umewapata watu 41,982,167 duniani kote na kuua 974,110, mwaka huu pekee.Rose anasema baada ya kuhangaika nao kwa muda mrefu na baadaye kupona kwa uthibitisho wa kitabibu, hivi sasa amejikita katika utafiti wa dawa hiyo iliyomponesha ili aweze kuwasaidia watu wengine wanaoteseka na Ukimwi.“Nimefi kia mahali pazuri, dawa yangu inaonesha matumaini na tayari imeshawasaidia watu ndani na nje ya nchi, ninachosubiri ni kibari cha serikali ili nianze kutibu watu.“Naishauri wizara ya afya inayoongozwa na mwanamke makini Ummy Mwalimu, ijikite kwenye utafi ti wa tiba asili, huku kuna matumaini makubwa.“Hapa nchini tunazo dawa nyingi sana za asili ambazo zinaweza kuwaponya watu na magonjwa mazito kama kansa, kisukari, presha na pumu.“Serikali iwaunge mkono watu wa tiba asili, tumeona kwenye Corona watu wanajifukisha, wanakunywa juisi ya malimao na kupata nafuu, tuache kupuuza tiba asili,” alisema Rose.Aliongeza kuwa, yeye anasimama kama shahidi wa tiba asili kwa sababu aliugua kiasi cha watu kumkatia tamaa, lakini amepona na sasa ameolewa na anaishi kwa furaha.“Hivi karibuni nilifanya ibada ya shukrani kwa Mungu kwa mema aliyonitendea, nimepona Ukimwi na nimepata mume, nifanye nini zaidi ya kumwinulia mikono Mungu wangu,” alisema Rose.

STORI: MWANDISHI WETU, RISASI
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger