8/09/2020

Aliyesaidiwa na Mkuu wa Majeshi atoa neno Baada ya Kuonekana na Kusajiliwa Jeshini


Mwanajeshi wa Kikosi cha Jeshi namba 833 Oljoro Arusha, Tete Mwaipaya, amemshukuru Mkuu wa Majeshi nchini Venance Mabeyo kwa kumpa nafasi ya kuingia jeshini kwa kuwa kabla ya nafasi hiyo alikuwa ni mwanasarakasi wa kucheza na  Baiskeli katika matamasha mbalimbali.

Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni wakati akifanya mazungumzo maalumu na EATV, na kusema kuwa nafasi hiyo aliitafuta kwa muda mrefu lakini hakuweza kuipata.


"Shughuli zangu zilikuwa ni hizi za Sarakasi nazunguka mikoa mbalimbali, kuna siku kulikuwa na sherehe Msasani Beach ya wanajeshi sasa alikuwepo Mkuu wa Majeshi pale nilionesha kipaji changu na ndipo alipoweza kuniona akasema huyu kijana aajiriwe jeshini" amesema Tete.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger